IQNA

Kuanza mashindano ya Qur’ani ya Sharja, Imarati

12:57 - November 20, 2008
Habari ID: 1710470
Mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu ya vituo vya kuhifadhisha Qur’ani katika Umoja wa Falme za Kiarabu yamenza katika mji wa Sharja. Mashindano hayo yanasimamiwa na Taasisi ya Qur’ani na Suna za Mtume SAW ya Sharja.
Mkuu wa Kamati ya Mashindano hayo Fauzi al Anzi amesema kuwa mashindano ya Qurani ya Sharja yanafanyika katika sehemu mbili ya wanawake na wanaume na yanawashirikisha wawakilishi wa vituo 49 vya Qurani vya miji mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Amesema kuwa washindani 130 wa kuhifadhi Qur’ani katika viwango na umri tofauti wanashiriki katika mashindano hayo yanayojumuisha kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Mkuu wa Kamati ya Mashindano ya Qurani ya Sharja amesema, lengo la kutayarishwa mashindano hayo ni kuimarisha moyo wa ushindani kati ya washiriki, kuhamasisha usomaji na kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kuelewa maneno ya Mwenyezi Mungu SW.
Amemalizia kwa kusema, washindi wa mashindano hayo watachaguliwa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu. 322706

captcha