Gazeti la Qatar la as-Sharq limeandika kwamba, jana makundi mawili ya vijana wa kike na kiume wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 20 walioshiriki kwenye mashindano hayo walisoma sura za Yunus na Hud, nalo kundi jingine la umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 likasoma sura za Ankabut na Rum. Mashindano hayo yameandaliwa na Idara Kuu ya Masuala ya Vijana ya Wizara ya Utamaduni ya Qatar. Sherehe za kufunga mashindano hayo zitafanyika siku ya Jumanne ijayo. 323770