Gazeti la Saudia la Ar-Riyadh limemnukuu Said bin Muhammad Makhayesh, mkuu wa elimu na malezi katika mkoa wa al-Makhwat ambako mashindano hayo yatafanyika akisema kuwa, mashindano hayo yatafanyika katika nyanja saba tofauti ambapo nyanja ya kwanza itakuwa ni kuhifadhi Qur'ani nzima kwa mbinu ya tajweed. Ameendelea kusema, hatua ya pili itakuwa ni kuhifadhi juzuu 20 kwa mbinu hiyohiyo ya tajweed, ya tatu itakuwa ni hifdhi ya juu 15, ya nne juzuu 10 na ya tano juzuu tano za kitabu hicho kitakatifu. Kundi la sita litakuwa ni la kuhifadhi juzuu ya 29 na 30 za Qur'ani na la saba litakuwa ni la kuhifadhi juzuu moja tu ambayo ni juzuu ya 30 ya kitabu hicho kwa mbinu hiyo hiyo ya tajweed.
Makhayesh amesema kuwa lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kuihudumia Qur'ani Tukufu na kuandaa uwanja unaofaa kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi kusoma na kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu. Ameongeza kuwa lengo jingine ni kuwafanya wanafunzi wawezi kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu. 323843