Ikiwa ni katika kuendeleza mfululizo wa vikao vyake kuhusiana na irfani katika dini za Kiyahudi, Kikristo na Kiislamu, Jumuiya ya Mazungumzi ya Dini ya Ufaransa imeandaa kikao maalumu kitakachojadili 'mazungumzo ya dini' hapo tarehe 26 Novemba katika ukumbi wa Pelloutier mjini Paris.