Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa lengo la kongamano hilo ni kuchunguza sheria zinazohusiana na wanawake katika nchi za Kiislamu na kuimarisha nafasi yao katika nyanja za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa.
Ajenda nyingine ya kongamano hilo ni kadhia ya kuwalinda wanawake kutokana na vitendo vya ukatili na ubaguzi na kutilia maanani suala la kuwaelimisha.
Kongamano la kwanza la Mchango wa Wanawake wa Kiislamu Katika Ustawi wa Nchi za Kiislamu lilifanyika Novemba 2006 katika mji wa Istanbul, Uturuki. 323974