IQNA

Wanawake wa Kikatoliki watembelea misikiti Uholanzi.

14:41 - November 24, 2008
Habari ID: 1712102
Wanawake wa Kikristo wa madhehebu ya Kikatoliki wa Uholanzi wameanza kutembelea misikiti ya Waislamu wa nchi hiyo. Mpango huo unasimamiwa na Jumuiya ya Wanahakati wa Kike ya Uholanzi.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa katika siku ya kwanza ya utekelezaji mpango huo, karibu wanawake 70 wa Kikristo wa Jumuiya ya Wanaharakati wa Kike wa Uholanzi walitembelea msikiti wa mji wa Utrecht.
Wanawake hao wa Kikatoliki walikutana na kufanya mazungumzo na maimamu wa misikiti na wanaharakati wa kike wa Kiislamu na kufafanuliwa misingi ya mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Maimamu wa misikiti ya Uholanzi vilevile walijibu maswali ya wanawake wa Kikatoliki kuhusu ada na sheria za Kiislamu, adabu na kanuni za kuingia msikitini na sheria za udhu na adhana za kabla ya Swala. 324438

captcha