Vijana wa kike na kiume wa nchi za Oman, Kuwait, Bahrain, Saudi Arabia na Qatar, walio na umri wa kati ya miaka 15 hadi 25 wameshiriki katika mashindano hayo kwa kuhifadhi sura za Yunus na Hud kwa mtindo wa Tajweed. Wengine wa umri wa miaka 10 hadi 14 walisoma hifadhi ya sura za Ankabut na Rum. Washiriki wa mashindano hayo pia wameshindana katika kuhifadhi hadithi 37 kutoka katika kitabu cha Riyadhu Swalihin cha Muhadith Nawawi. Pambizoni mwa mashindano hayo, washindani walikitembelea kituo cha utamaduni wa Kiislamu cha Fanar katika mji wa Doha, ambao ni mji mkuu wa Qatar. Katika upande wa pili, Khalid Yusuf al-Malla Mkuu wa Idara Kuu ya Masuala ya Vijana wa Qatar ambaye pia ni katibu wa mashindano hayo ya kimataifa ametagaza kwamba, sherehe rasmi za kufunga mashindano hayo zitafanyika leo Jumanne. Amesema washindi watapewa zawadi pamoja na loho za kuwashukuru kwa kushiriki katika mashindano hayo. 324956