Kwa mujibu wa shirika la Isesco, Abdul Aziz Othman al Tuweijiri Katibu Mkuu wa shirika hili amesema katika kikao cha ‘Vijana wa Ulimwengu wa Kiislamu, Fursa Zilizopo na Changamoto za Baadaye’ huko Tunis Tunisia kwamba, kuzingatia masuala yanayowahusu vijana katika Nyanja tofauti zikiwemo za elimu, ajira, kushajiishwa misimamo ya wastani, usamehevu na utamaduni wa mazungumzo kunapaswa kupewa uzito katika mipango ya serikali za nchi za Kiislamu. At-Tuweijiri amesisitiza kwamba ni kwa kutekelezwa mipango hiyo tu ndipo nchi za Kiislamu zinaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana katika mustakbali wao. Pia ametaka mwaka wa 2009 utajwe kuwa mwaka wa vijana wa ulimwengu wa Kiislamu na kushirikishwa vijana hao katika mipango mbalimbali ya serikali kuhusiana na vijana. Ametoa ripoti fupi inayohusiana na mipango iliyotekelezwa kwa ajili ya kutajwa mji wa Qeirawan kuwa mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu mwaka ujao na pia kikao cha Mawaziri wa Mazingira wa nchi wanachama wa OIC kinachatazamiwa kufanyika mwaka 2010 huko Tunisia. 325678