IQNA

Kikao cha Uwekezaji wa Kiislamu kufanyika Malta

11:44 - November 27, 2008
Habari ID: 1713186
Kikao cha kimataifa cha uwekezaji wa Kiislamu kitafanyika huko Malta tarehe 28 Novemba kwa ushirikiano wa taasisi ya wakurugenzi, jumuiya ya wenye mabenki na muungano wa waajiri nchini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa di-ve , washiriki wa semina hiyo watakuwa ni pamoja na wahasibu, wanabenki, maajenti na maafisa wa uwekezaji pamoja na baadhi ya wanachuo.
Ajenda kuu ya kikao hicho itakuwa ni kujadili njia ya kustawisha taasisi za uwekezaji kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Abdullah As-Shami mhadhiri wa sheria za Kiislamu na Robin Batigig Mkuu wa Taasisi ya Ukurugenzi ya Malta ni miongoni mwa watu watakaohutubia semina hiyo.
326416
captcha