Jaji Mkuu wa Palestina Sheikh Taysir al Tamimi, Muhammad Sulaiman al Dujani muasisi wa kituo cha Mwenendo wa Wastani wa Uislamu huko Palestina na wanazuoni na Kiislamu na Kikristo wanashiriki katika kongamano hilo.
Sheikh Taysir al Tamimi amesema katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwamba dini ya Kiislamu inawalingania wafuasi wake kufuata njia nyoofu, kufanya mazungumzo yenye lengo na kujiepusha na upotofu na kufurutu mipaka katika fikra.
Ameashiria kwamba Uislamu ni dini ya dunia nzima iliyokuja na mwenendo wa wastani na kujiepusha na kuchupa mipaka na amewataka wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu kufafanua thamani na matukufu ya dini hiyo.
Sheikh al Tamimi amesema kuwa misingi na itikadi za Uislamu zinasisitiza juu ya msimamo wa wastani na kujiepusha na misimamo ya kimakundi na kwamba Qur'ani Tukufu na suna za Mtume Muhammad SAW pia zimetilia mkazo suala hilo la msimamo wa wastani hata katika masuala ya ibada.
Amemalizia kwa kusema, Uislamu umewataka waumini kujiepusha na israfu na ubadhirifu na kutoa kwa njia za busara.
Makala mbalimbali zimewasilishwa katika kongamano hilo la "Uislamu, Dini ya Wastani'. 326248