IQNA

Ufaransa kutangaza Idul Adh’ha sambamba na Saudi Arabia

17:10 - November 29, 2008
Habari ID: 1713928
Baraza la Waislamu la Ufaransa CFCM lilitangaza jana Ijumaa kwamba Jumatatu tarehe 8 Disemba itaadhimishwa nchini humo kama sikukuu ya Idul Adh’ha sambamba na Saudi Arabia.
Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo, Waislamu wameombwa kuzingatia viwango na masuala ya afya katika siku hiyo na kuchinja kondoo kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Mara hii idadi kubwa ya Waislamu wa Ufaransa wanajiandaa kukukaribisha sherehe za siku hii muhimu katika kalenda ya Kiislamu na hivyo kuongeza idadi ya vichinjio vya wanyama nchini nchini humo katika siku hiyo ya furaha na shangwe. 327166
captcha