IQNA

Nchi za Magharibi zinataka kuwagonganisha Waislamu

17:05 - November 29, 2008
Habari ID: 1713929
Mbegu ya misimamo ya kupindukia na kupindukia mipakana imepandwa katika nchi na jamii za Kiislamu na nchi za Magharibi ili kuwagonganisha Waislamu na kuwafanya waendelee kuishi katika hali ya maradhi hayo hatari.
Misimamo kama hiyo na vilevile usufi ni maradhi makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu, maradhi ambayo yamezushwa na kulelewa na maadui wa Uislamu wa nchi za Magharibi. Hayo yamesemwa na Sheikh Idriss, mwakilishi wa Sudan katika kikao cha kwanza cha ‘fikra ya pamoja ya wanachuo wa ulimwengu wa Kiislamu.’ Amesema, hali ya machafuko yanayoendelea hivi sasa nchini Iraq ni mfano wa wazi wa kufurutu mipaka katika fikra za kidini. Akizungumza katika siku ya pili ya kikao hicho, chini ya anwani ‘uadui wa Magharibi dhidi ya Uislamu’, Sheikh Idrsiss amesisitiza kuwa jamii nyingi za kiraia za Magharibi zina matatizo na Uislamu na kwamba mabeberu wa nchi hizo wana matatizo na shaka katika kuamiliana na Waislamu. Amesema kuwa, kutekwa na kukaliwa kwa mabavu Sudan na nchi nyinginezo za Kiislamu kulitokana na masuala ya kidini ambayo yameashiriwa pia katika Torati na Injili. Amesema, serikali na watawala wa Kiislamu wanapasa kutanabaishwa na kushajiishwa wachukue hatua za dharura za kuzuia maadui kumwagwa ovyo damu ya Waislamu. 326987
captcha