IQNA

Mashindano ya kimataifa ya wanajeshi nchini Saudi Arabia

11:45 - November 30, 2008
Habari ID: 1714105
Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanajeshi yatafanyika huko Riadh mji mkuu wa Saudi Arabia katoka tarehe Mosi Aprili hadi 17 mwezi huohuo.
Gazeti la ar-Raya la nchini Qatar limeandika kuwa, Muhammad Arid AbduRaheem, Katibu wa duru ya 12 ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kwa wanajeshi amesema kuwa mashindano hayo ya Saudi Arabia yatawashirikisha wanajeshi wa nchi za Kiislamu na kufanyika kwa muda wa siku 16. Ameishukuru Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar kwa kuandaa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kwa wanajeshi wa nchi hiyo na kusema kuwa, hiyo ni hatua nzuri katika kueneza mafundisho ya Qur'ani katika matabaka yote ya jamii ya nchi hiyo. Mwishoni mwa mashindano hayo ya Qatar walioshinda walipewa zawadi nono pamoja na loho za shukrani kwao kwa kushiriki katika mashindano hayo. Wakati huohuo washiriki wote wa mashindano yaliyotajwa walishajiishwa kushiriki katika mashindano yajayo ya kila mwaka ya Qur'ani kwa kupewa fursa ya kushiriki katika ibada muhimu ya hija ya huko Makka.
Duru ya 12 ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanajeshi wa Qatar yalifanyika tarehe 2 hadi 6 Novemba ambapo wahifadhi 58 walishiriki katika mashindano hayo katika makundi 6 ya kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 20, juzuu 15, juzuu 10, juzuu tano na juzuu moja ya kitabu hicho kitakatifu. 327228
captcha