IQNA

Vikao vya Kiislamu vinapasa kutangazwa zaidi

11:44 - November 30, 2008
Habari ID: 1714106
Matangazo na upashaji habari wa kutosha unapasa kufanyika kuhusiana na warsha na vikao vya Kiislamu kikiwemo cha wanachuo wa Kiislamu, ili washiriki wengi zaidi wapate kushiriki katika vikao hivyo na wakati huohuo kuwapa fursa ya kuweza kujiandaa vyema kabla ya kushiriki katika vikao kama hivyo.
Hayo yamesemwa na Arafat Daniz, mwanachama wa Jumuiya ya Urafiki Baina ya Dini na Tamaduni ya Uturuki na mshiriki wa kikao cha kwanza cha 'fikra ya pamoja ya wanachuo wa ulimwengu wa Kiislamu' kilichomalizika hivi karibuni mjini Tehran. Akizungumza na shirika la IQNA Dazin ameelezea kufurahishwa kwake kutokana na kupata fursa ya kushiriki katika kikao hicho na kuongeza kwamba, vikao kama hivyo vinawafanya Waislamu kujuana zaidi na hivyo kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao kama inavyofundisha dini tukufu ya Kiislamu. Mwanachuo huyo wa Uturuki amesema, kama walivyo watu wengi duniani, alikuwa ameathirika na kupotoshwa na propaganda sumu zinazoenezwa na vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini hivi sasa amepata sura halisi ya Waislamu wa Iran baada ya kuitembelea nchi hii na kushiriki katika kikao kilichotajwa. Amewataka waandaaji wa kikao hicho kuandaa vikao vingine kama hivyo kwa wasomi na wahandisi wa Kiislamu ili kuwawezesha kupata sura halisi ya Iran na hivyo kuimarisha umoja na mshikamano wa Waislamu ulimwenguni. Dazin amesema kuwa, lengo kuu la wanachuo wa Kiislamu ni kuhubiri mafundisho halisi ya Uislamu miongoni mwa watu na kuleta umoja kati ya Waislamu. Amesema, matatizo yote yanayowakumba Waislamu hii leo yanatokana na hitilafu na mgwanyiko wao ambao kimsingi unatokana na upuuzaji wao wa mafundisho ya Uislamu. Amesema, tatizo hilo linaweza kutatuliwa tu kwa kunyanyua kiwango cha elimu na maarifa ya Waislamu kuhusiana na dini yao. 327090
captcha