Naibu Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Hisham al Abbas amesema kwamba ajenda ya kongamano hilo ni kuchunguza maana ya ‘uwezo’ wa kwenda kuhiji, uwezo wa wahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu wa kutekeleza ibada za Hija kwa mujibu wa falsafa ya fiqhi na hali halisi ya zama hizi na kuarifisha maeneo matakatifu ya Makka na Madina.
Al Abbas amesema, kongamano hilo pia litajadili na kufafanua misingi ya sheria za Kiislamu kuhusu ibada ya Hija, upande wa kibinadamu na kijamii wa amali na matendo ya Hija na fatuwa zilizotolewa na wanazuoni kuhusu uwezo wa wahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 328460