Akademia hiyo imeanzishwa kwa shabaha ya kuwafunza mahujaji amali na ibada ya Hija, kuwatayarisha kwa ajili ya kutekeleza ipasavyo ibada hiyo na kuzuia tabia ya baadhi ya wafanya biashara wanaotumia vibaya msimu huu wa Hija kwa maslahi yao binafsi.
Vilevile kituo hicho cha Kiislamu kilichoko mjini Paris kinatoa mafunzo kwa mahujaji kuhusu namna ya kulinda usalama wao mbele ya hatari za aina yoyote.
Mkurugenzi wa akademia hiyo Zakaria Na'na' amesema kuwa kituo hicho kinatoa mafunzo kwa mahujaji kuhusu hatua za kimafya za baadhi ya makundi na kutoa huduma mbalimbali.
Na'na' amesema kuwa mwaka jana karibu mahujaji elfu arubaini walikwenda Makka kuhiji na kwamba elfu saba kati yao walikuwa na viza bandia na wengine hawakuridhishwa na mazingira ya safari yao.
Euro milioni 250 hutumika kuwahudumia mahujaji wa Ufaransa katika ibada ya Hija na Waislamu elfu 40 wa nchi hiyo huenda kuhiji Makka kila mwaka. 328944