IQNA

Imam Khomeini (SA) ndiye muasisi wa harakati ya Hizbullah

11:28 - December 04, 2008
Habari ID: 1715704
Mkuu wa Idara ya Hija ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Muhammad Yazbak, amesema kuwa hayati Imam Khomeini ndiye muasisi wa mkakati wa harakati hiyo. Amesisitiza pia juu ya udharura wa kulinda harakati ya mapambano ya Hizbullah katika kukabiliana na fitina za maadui.
Kwa mujibu wa Jarida la Lubnan Alan , Sheikh Muhammad Yazbak ambaye ni mwanachama wa Baraza Kuu la chama cha Hizbullah na Mkuu wa Idara ya Hija ya chama hicho amesema hayo katika mkutano wake na Ayatullah Muhammad Muhammadi Reyshahri, Mwakilishi wa Waliul Faqih na Mkuu wa Idara ya Mahujaji Wairani. Sheikh Yazbak amongeza kuwa: Lengo la Imam Khomeini la kutaka Wapalestina waondoke katika makucha ya Waisraeli litafikiwa kwa kufuata miongozo na usimamizi wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu”.
Ameongeza kuwa Walebanon hawataruhusu harakati ya mapambano isamabaratishwe kutokana na migongano ya ndani. ‘Hii ni kwa sababu maadui daima wanazusha fitina na sisi tutaendelea na mkakati pamoja na stratijia aliyotuainishia Imam Khomeini’ amesema mwanachama huyo wa Hizbullah.
Sheikh Muhammad Yazbak amemaliza kwa kusema: “Sisi tunajifakharisha kuwa wanajeshi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kuutetea Uislamu halisi na mkono wa Wilaya ya Ahlul Bayt”. 329608
captcha