Kwa mujibu wa Muhammad Abdu Raheem, mmoja wa viongozi wa Baraza la Mji wa Nablos, askari hao wa Kizayuni waliandika maandishi hayo ya dhihaka katika kuta za misikiti ya vijiji kadhaa vya viunga vya mji wa Nablos na Ramallah. Maandishi hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiibrania yalikuwa yakimtusi Mtume Muhammad (saw) na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Vilevile kwa kuandika neno 'Hebron', ambalo linatumiwa na Mayahudi wenye misimamo ya kupindukia kwa maana ya kufukuzwa Wapalestina kutoka kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, kwenye kuta za misikiti, Wazayuni hao wanachochea kufukuzwa kwa Wapaletina wote wanaoishi katika eneo hilo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Inakumbushwa hapa kwamba, Jumatatu usiku Wapalestina 16 waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga kufukuzwa Wapalestina kutoka kwenye nyumba zao walijeruhiwa vibaya na askari hao wa Kizayuni. 329333