Nasir Jauda amesema kuwa Jordan inalaani kitendo chochote kinachovunjia heshima maeneo matakatifu ya mji wa Quds. Amesema kuwa hatua hiyo itaamsha hasira za Waislamu na kwamba haiwezi kuhalalishwa kwa njia yoyote ile.
Waziri wa Habari wa Jordan ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kuzuia hatua kama hizo na kuihimiza jamii ya kimataifa kufanya juhudi za kukabiliana na vitendo vya Israel vya kuvunjia heshima maeneo matakatifu ya Kiislamu. 330048