Kwa mujibu wa ripoti ya IQNA kutoka Jordan, Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jordan Nasir Jaudah amesema: "Jordan inapinga hatua yoyote ya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kuhusiana na kitendo cha Mayahudi kuingia Msikiti wa al Aqsa, Israel ndio inayobeba jukumu la kuvunjiwa heshima msikiti huo na matokeo yoyote hatari yatakayofuatia tukio hilo".
Ameongeza kuwa hatua hizo za utawala ghasibu wa Israel zinaenda kinyuma na sheria za kimataifa kuhusu wadhifa wa utawala huo ghasibu kama mvamizi.
Nasir Jaudah amewataka wakuu wa Israel kusitisha vitendo vya kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuzuia sera hizo za Wazayuni za kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa lengo la kuchochea hisia za Waislamu. Amesema, uchochezi huo wa Waisraeli utaathiri vibaya mchakato wa kutafuta amani katika eneo la Mashariki ya Kati. 330202