Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait la Al Qabas, wakuu wa shule hiyo katika mji wa Brisbane wamepinga kuimbwa wimbo huo ulio dhidi ya Uislamu wenye anwani ya "Ewe Australia, Endelea na Uadilifu". Mkuu wa zamani wa shule hiyo la Kiislamu ya Brisbane, Parveen Chand, amesema kuwa uongozi wa shule unasema, wimbo huo wa taifa unaenda kinyume na mafunzo pamoja na misingi ya dini ya Kiislamu na hivyo umepigwa marufuku shuleni hapo.
Wiki iliyopita, karibu Waustralia 300 wenye misimamo ya kufurutu mipaka walijumuika katika mji wa Gold Coast wa nchi hiyo na kupinga utolewaji leseni ya kujengwa shule mpya za Kiislamu nchini humo.
Waandamanaji wamedai kuwa kuasisiwa shule mpya za Kiislamu nchini humo kutaibua mgawanyika katika jamii ya nchi hiyo. 330507