Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya Miana nchini Iran Hujjatul Islam Ali Asghar Sayyadi ambaye ameongeza kuwa, ni wajibu wa wakuu wa idara mbalimbali kuhuisha swala za jamaa. Sheikh Ali Asghar amesema, wakuu wa idara mbalimbali wanatarajiwa kuwa mstari wa mbele wa swala za jamaa na kuwa kigezo cha kuigwa na wafanyakazi wengine.
Hujjatul Islam Ali Asghar Sayyadi ameashiria aya na hadithi zinazohimiza swala za jamaa na akasema: Swala za jamaa ni nembo ya umoja na mshikamano wa Kiislamu. 331025