IQNA

Kisomo cha dua ya Arafa leo nchini Zambia

10:40 - December 08, 2008
Habari ID: 1717159
Kisomo cha dua ya Arafa kinafanyika leo nchini Zambia katika shughuli inayosimamiwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
Kikao cha kisomo cha dua ya Arafa kilitarajiwa kuanza saa nne na nusu asubuhi kwa wakati wa Zambia kwa kufunguliwa na kisomo cha Qur'ani Tukufu. Shughuli hiyo itaendelea hadi wakati wa swala ya Magharibi.
Lengo la shughuli hiyo ya kimaanawi na kiroho limetajwa kuwa ni kufafanua mafundisho aali ya Kiislamu kwa Waislamu wa Zambia.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Zambia Hujjatul Islam Asadi Muwahhid amesema kuwa katika shughuli hiyo Waislamu wa Zambia watajifunza maana na mafunzo ya tauhidi yaliyomo katika dua ra Arafa ambayo imepokelewa kutoka kwa Imam Hussein bin Ali (as) mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (saw).
Asadi amesema kuwa moja ya ajenda ya shughuli hiyo ni hotuba zitakazozungumzia maudhi ya 'Siku ya Arafa na nafasi ya siku hiyo muhimu katika Uislamu na Qur'ani" na "Falsafa ya Waislamu kuhudhuria katika uwanja wa Arafa huko Saudi Arabia."
331049
captcha