IQNA

Kimya kuhusu masaibu ya Palestina, mwanzo wa kulegeza msimamo

10:27 - December 09, 2008
Habari ID: 1717400
Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah, mwanachuoni mwandamizi wa Mashia nchini Lebanon amekosoa kimya cha nchi za Kiarabu na Kiislamu mbele ya mkasa wa mzingiro wa Gaza na kadhia nzima ya Palestina na kukitaja kimya hicho kuwa batili, kuanguka katika mtego na mwanzo wa kusalimu amri.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Makka, Allamah Fadhlullah ameyasema hayo alipokutana na wasomi wa kidini na wanasiasa katika idara yake ya Hija katika mji mtakatifu wa Makka. Katika mkutano huo, ameonya pia kuhusu tangazo la baadhi kuwa wako tayari kufanya mazungmzo na adui (Mzayuni) kwa lengo la kuwa na uhusiano wa kawaida. Amesema, hatua kama hiyo itakuwa ni kulishinikiza na kulidhulumu taifa la Palestina ambalo tayari limedhulumika.
Mwanachuoni huyo mwandamizi wa Kishia nchini Lebanon amesema kuwa: "Umma wa Kiislamu unapaswa kuwa Umma mmoja ili uweze kuamua hatima ya dunia". Amesema, dola kubwa la Kiislamu duniani linaweza kuasisiwa kwa kutumia suhula na utajiri uliopo katika nchi za Kiislamu hasa kawi pamoja na idadi ya watu iwapo Mashia na Masuni wataungana. 331596
captcha