IQNA

Sarkozy alaani hujuma dhidi ya makaburi ya Waislamu Ufaransa

15:51 - December 10, 2008
Habari ID: 1717831
Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amelaani hujuma na mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya makaburi ya Waislamu ya eneo la Norte-Dame de Lorette huko kaskazini mwa nchi hiyo.
Gazeti la Peninsulaqatar limeripoti kuwa Rais wa Ufaransa amesema kuwa, shambulizi hilo dhidi ya makaburi ya Waislamu ambalo ni la tatu kufanyika nchini humo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, ni dalili ya ubaguzi na hisia za chuki dhidi ya jamii ya Waislamu wa Ufaransa.
Mwendesha Mashtaka wa Ufaransa amewaambia waandishi wa habari kwamba karibu makaburi 500 kati ya makaburi 576 ya Waislamu ya eneo la Norte-Dame de Lorette yalivunjwa Jumapili iliyopita sambamba na kuwadia sikukuu ya Idul Adh'ha. Amesema kuwa, polisi inawasaka watu waliohusika la kitendo hicho.
Aprili mwaka huu makaburi mengine 148 ya Waislamu katika eneo la makaburi ya wanajeshi wa Kiislamu wa Ufaransa yalishambuliwa na kuharibiwa. 332132
captcha