IQNA

Wakuu wa Hizbullah wakataa kukutana na Carter

12:54 - December 11, 2008
Habari ID: 1717946
Viongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamekataa ombi la kufanya kikao na Jimmy Carter rais wa zamani wa Marekani aliye safarini nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, Rick Jafculca Msemaji wa Carter amesema viongozi wa harakati ya mapambano ya Hizbullah wamesema hawako tayari kukutana na Carter.
Wakati huo huo Jimmy Carter amesema, ameelewa kuwa viongozi wa Hizbullah hawatakuna na rais au kiongozi yeyote wa sasa na wa zamani wa Marekani. Carter hata hivyo amesema kuwa atakutana na viongozi wengine wa Lebanon.
Safari ya Carter nchini Lebanon itafuatiwa na safari katika nchi jirani ya Syria. Akiwa Damascus anatazamiwa kukutana na Rais Bashar al Asad wa Syria na viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina, Hamas.
332324

captcha