IQNA

'Wiki ya Gaza' kufanyika katika vyuo vikuu 100 Ulaya

12:42 - December 11, 2008
Habari ID: 1717951
Raia wa Bara Ulaya wanaopinga mzingiro wa Ukanda wa Gaza unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel wameandaa 'Wiki ya Gaza' kwa lengo la kuwazindua wakazi wa bara hilo kuhusu masaibu ya Wapalestina hasa wakazi wa Gaza.
Kwa mujibu wa Arafat Ma'dhi, Mwenyekiti wa Kundi la wakazi wa Ulaya wanaotaka kukomeshwa mzingiro wa Gaza amesema: 'Wiki ya Gaza itafanyika mwezi Februari mwakani katika vyuo vikuu 100 barani Ulaya'. Amesema, kati ya harakati za wiki hiyo ni kuonyesha taswira za matatizo na masaibu ya watu wa Ukanda wa Gaza pamoja na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mwanaharakati huyo wa Kiislamu amesema kuwa Umoja wa Ulaya haujachukua hatua zozote za maana kuhitimisha mzingiro wa Gaza. Amesema, nchi za Ulaya hazijaushinikiza utawala wa Kizayuni kusitisha hatua zake zilizo dhidi ya binadamu na za kidhalimu huko Palestina.
Arafat Ma'dhi amesema mzingiro wa Gaza ni kinyume cha sheria na kanuni zote za kimataifa. 332384
captcha