Katika taarifa hiyo, chama cha Hizbullah kimekemea vikali uchokozi na hujuma ya askari wa utawala huo dhidi ya matukufu ya Kiislamu, ikiwemo misikiti ya Ufukwe wa Magharibi na kusema kuwa, vitendo vya dharau vya utawala huo dhidi ya matukufu ya Waislamu vimekuwa vikiongezeka baada ya mazungumzo ya kidini huko mjini New York Marekani.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Hizbullah imelaani vikali hatua za kigaidi za Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina, uporaji wa mali zao na dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu katika Ufukwe wa Magharibi na kusisitiza kwamba, utawala huo umekuwa ukikiuka wazi haki za Waislamu kwa kadiri kwamba, hivi sasa unatoa ruhusa ya kutusiwa Mtume Mtukufu (saw) na kuvunja heshima ya misikiti bila ya woga wowote.
Huku ikielezea kushangazwa kwake na kimya cha kimataifa kuhusiana na jinai zinazotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina na hasa baada ya kumalizika mazungumzo yanayotajwa kuwa ni ya kidini huko New York, Hizbullah imesisitiza kwamba, kuheshimiwa matukufu ya kidini ambako kumesisitizwa katika sheria za kimataifa kunapaswa kuheshimiwa na wote. Imesema kwa kuzingatia suala hilo, jamii ya kimataifa inapasa kusimama na kukabiliana na jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel huko katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina. 332352