Ayatullah Qarebaghi amesema kuwa vitisho au hata mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya nchi za Kiislamu hayawezi kuitokomeza dini hiyo na kwamba sera zao za kijeshi zinawazindua zaidi walimwengu na kuwafanya wawe macho kuhusu njama za nchi hiyo. Mwanazuoni huyo amesisitiza kuwa tatizo kubwa la wakati huo ni watu ambao wamevaa vazi la Uislamu na wanalitumia vazi hilo dhidi ya dini hiyo tukufu.
Ameashiria mchango wa maulama katika kueneza mafundisho ya Kiislamu na akatahadharisha juu ya njama za maadui wanaoeneza propaganda chafu dhidi ya madhehebu ya Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw). 332483