IQNA

Haki ya kujieleza ni msingi wa haki za binadamu

15:31 - December 15, 2008
Habari ID: 1719487
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti nchini Iran Muhammad Hashimi amesema kuwa, mwanadamu ambaye ni kiumbe kitukufu, ana hadhi kubwa na kwa msingi huo anapaswa kupewa heshima anayostahiki.
Muhammad Hashimi ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa kieneo wa "Haki na Utukufu wa Mwanadamu Katika Mtazamo wa Qur'ani Tukufu" amesema, haki ya kujieleza ni moja kati ya haki za kimsingi za mwanadamu. Amesema kuwa, inasikitisha kuona kwamba baadhi ya nchi hazitoi kipaumbele kwa mjadala wa haki ya kujieleza.
Muhammad Hashimi amesisitiza kwamba uhuru wa fikra ni katika haki muhimu za mwanadamu na kwamba haki hiyo pamoja na ile ya kujieleza ni dalili za ubinadamu wa mwanadamu.
Ameashiria mchango wa Mitume wa Mwenyezi Mungu katika kuimarisha misingi ya haki na utukufu wa mwanadamu na akasema: Vitabu vya Mitume hao pia vimesisitiza mno juu ya udharura wa kuheshimiwa haki na utukufu wa binadamu. 333358


captcha