Akizungumza hivi karibuni, Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah amesema, msaada wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel katika vita vyake dhidi ya Lebanon ulifanyika katika hali ambayo viongozi wa Washington walidai kuwa, hawana chuki na Walebanoni. Amesema: Wamarekani waliisaidia Israel katika kuharibu miundo mbinu ya Lebanon na kuwaua mamia ya watoto, wanawake na wazee nchini humo. Aidha amesema Wamarekani waliwasaidia Wazayuni kwa mabomu ya vishada ambayo yanaendelea kuhatarisha maisha ya Walebanoni hadi leo. 335772