Hiyo ni kauli ya majaji katika Mashindano ya pili ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yaliyofanyika hapa Tehran hivi karbuni.
Katika mashiundano hayo, majaji mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu kama vile Abu- Einein She'isha kutoka Misri ambaye alikuwa msimamizi wa mashindano, Hassan Hamdan wa Lebanon, Abdulbasit Imam Tumara kutoka Ufilipino, Ahmad Naina na Hilmi Jamal kutoka Misri.
Hassan Hamadan amesema kuwa mashindano yanayoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na nafasi ya juu ya Qur'ani miongoni mwa viongozi, wanachuo na wananchi Waislamu wa Iran ni jambo linaloashiria ukweli huo. Amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uzoefu wa muda mrefu na unaonawiri katika kuandaa mashindano ya Kiislamu na ya Qur'ani. Amesema kuwa suala hili linaifanya Iran kuwa mwenyeji bora zaidi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo.
Naye Ahmad Nai'na qari mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu na aliyekuwa mmoja kati ya majaji katika mashindano ya kimataifa ya wanachuo wa Kiislamu ya Tehran anaamini kuwa njia ya muafaka ya umma kunufaika na Qur'ani ni kuihifadhi, kuisoma, kutafakari na kufanya utafiti kuhusu mafunzo yake. Amesema kuwa mbali na kuandaa mashindano ya qiraa au kusoma na kuihifadhi, kunapaswa kuwepo mikakati ya kuandaa mashindano ya ufahamu wa Qur'ani tukufu.
Kwa upande wake Mohammad Hussein Ad-Daumana , hafidh wa Qur'ani kutoka Syria ambaye alikuwa amepangwa kuwa katika kamati ya majaji katika Mashindano ya pili ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu ametoa mapendekezo ya kuandaliwa kwa njia bora zaidi mashindano ya kimatiafa ya Quran. Amesema: Kila mwaka baada ya kumalizika mashindano ya Qur'ani kunapaswa kufanyika uchunguzi wa maoni ya majaji na washiriki ili kubaini nuka dhaifu za mashindano kwa lengo la kuzirekebisha. Aidha qari huyo ya Syria ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kumenzi Ustadh Abu- Einein She'isha wa Misri na kusema, Ustadh She'isha ni kigogo katika maqari wa Qur'ani duniani hivi sasa.
Itakumbukwa kuwa Mashindano ya Pili ya Kimatiafa ya Qur'ani ya Wanachuo yalifanyika Novemba 10-14 mjini Tehran na kuwashirikisha maqari na mahafidh kutoka zaidi ya nchi 42. 335854