IQNA

Waislamu Ufaransa waandamana kulaani kuchomwa msikiti Lyon

12:36 - December 21, 2008
Habari ID: 1720965
Msikiti wa eneo la Saint-Priest ulioko kwenye viunga vya mji wa Lyon nchini Ufaransa umechomwa moto na kusababisha hasara katika kitendo cha jinai kilichofanyikwa kwa makusudi.
Kitendo hicho kimezusha hasira kubwa za vyama vya siasa na jamii ya Wislamu ya Ufaransa ambayo imesema, ni ishara ya kuongezeka wimbi la uhasama na chuki za kibaguzi dhidi ya dini ya Kiislamu.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imethibitisha kutokea kitendo hicho ambacho imesema kuwa ni cha makusudi, kiovu na ambacho hakiwezi kuvumulika. Taarifa ya wizara hiyo imesema: Moto uliotokea kwenye msikiti wa Saint-Priest katika viunga vya mji wa Lyon umesababisha madhara na kuchoma vitabu kadhaa vya kidini.
Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu la Ufaransa Muhammad Musawi amelaani vikali kitendo hicho kiovu la kuitaka serikali ya Paris kuwatia nguvuli wahusika. Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufansa Michele Alliot-Marie ameeleza kusikitishwa na kitendo hicho na kusema kuwa polisi imeanza uchunguzi wa kujua nani walihusika na tukio hilo la kuchoma moto msikiti.
Maandamano makubwa yamepangwa kufanyika leo Jumapili mbele ya msikiti huo kupinga vitendo viovu na vya kibaguzi vinavyowalenga Waislamu nchini Ufarasa. Siku chache zilizopita makaburi karibu mia tano ya Waislamu yalishambulia na kuvunjwa na watu wasiojulikana huko kaskazini mwa Ufaransa. Vilevile mwezi Agosti mwaka huu msikiti wa Mizyu huko mashariki mwa nchi hiyo ulishambuliwa na watu wasiojulikana. 336086

captcha