IQNA

Kikao cha "Nafasi ya Waislamu katika kukabiliana na Ugaidi"

12:17 - December 21, 2008
Habari ID: 1720967
Kikao cha nafasi ya Waislamu katika kukabiliana na ugaidi kimefanyika New Delhi na kuhudhuriwa na wasomi mbalimbali wa Kiislamu wa India.
Kwa mujibu wa gazeti la India Daily, kikao hicho kinafanyika kwa lengo la kuuarifisha Uislamu kama dini inayopinga ugaidi na utumiaji mabavu.
Sheikh Muhammad Madani, Kiongozi wa Jumuiya ya Maulama wa India amesema: Kongamano hilo pia litawashukuru Waislamu wa India kwa kujitokeza kwa wingi kupinga matukio ya kigaidi yaliyojiri hivi karibuni mjini Mumbai. Amesema tuhuma dhidi ya Waislamu hazina msingi wowote kwa sababu iwapo Waislamu walishiriki katika ugaidi huo basi hawangejitokeza kwa wingi kuulani.
Shabana Azmi mcheza filamu mashuhuri wa India alishiriki pia katika kongamano hilo na kutangaza kuwa, Waislamu wanapaswa kufanya juhudi zaidi kuthibitisha kuwa Uislamu unapinga ugaidi.
335785

captcha