IQNA

Sera za Marekani, chanzo cha kuenea misimamo mikali duniani

11:53 - December 21, 2008
Habari ID: 1720969
Sera potofu za Marekani na waitifaki wake wa Ulaya katika masuala ya kimataifa hasa kadhia ya Palestina na kuunga mkono ubaguzi wa rangi na ukatili wa utawala wa Kizayuni ndio chanzo cha kuenea misimamo mikali ya kidini na ugaidi duniani.
Kwa mujibu wa gazeti la al Akhbar la Misri Abrus Baldisera mtaalamu wa maswala ya mashariki amesema kuwa nchi za Kiarabu hivi sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi za kimatiafa kama vile kughusubiwa ardhi za Wapalestina na utawala wa haramu Israel ambao unatekeleza sera za kibaguzi.
Ameongeza kuwa, "nchi za Magharibi zina misimamo ya kindumakuwili kuhusiana na matatizo ya dunia jambo ambalo limeibua migogoro duniani. Wamagharibi wamewasilisha mpango wa mazungumzo ya kidini kama chombo tu cha kuendeleza malengo yao ya kibeberu".
Profesa Abrus Baldisera amesema kuwa, wataalamu wa masuala ya mashariki hawapaswi kuathiriwa na mitazamo na fikra za sera za Kimagharibi bali wanapaswa kuwa huru katika utafiti wao. 335767
captcha