IQNA

Qur’ani, msingi halisi wa hadhi na utukufu wa Waislamu

12:34 - December 21, 2008
Habari ID: 1721009
Matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu yatatatuliwa kwa kushikamana barabara na Qur’ani, na kitabu hicho ndiyo chanzo halisi cha utukufu na hadhi ya umma wa Kiislamu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Teolojia ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Gaza huko Palestina Nasiim Yasin katika kongamano la Qur’ani Tukufu na Mchango wa Wake Katika Kutatua Matatizo ya Umma wa Kiislamu. Nasiim Yasin amesema: Maulama, walinganiaji na watafiti wa Kiislamu wanaweza kutumia mafundisho na misingi ya Qur’ani Tukufu kutatua matatizo na masuala mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.
Amesisitiza pia juu ya kufanyika utafiti zaidi kuhusu muujiza wa kielimu wa Qur’ani Tukufu. Amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kusisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhi, kufasiri na kusoma Qur’ani Tukufu, kufafanua muujiza wa kielimu wa kitabu hicho na kuimarisha utamaduni wa kufunza na kujifunza maarifa ya Qur’ani. 335622
captcha