IQNA

Benki za Kiislamu zanusurika na mgogoro wa fedha duniani

14:21 - December 23, 2008
Habari ID: 1721897
Benki za Kiislamu zimenusurika na mgogoro wa fedha duniani kwa sababu zinafuata misingi ya sheria za Kiislamu.
Gazeti la Arab News la Saudi Arabia limemnukuu Mkuu wa Halmashauri ya Kiislamu ya Ustawi wa Sekta Binafsi ICD Khaled Al-Aboodi akisema kuwa: "Benki za Kiislamu zinazingatia kwa kina Sheria za Kiislamu na zinadhibitiwa na Bodi za kitaalamu". Ameongeza kuwa benki zinazozingatia sheria za Kiislamu haziruhusiwa kutoa mikopo yenye riba ziada yaani inayochukua muda mrefu kulipwa (sub prime loans). Afisa huyo mwandamizi wa sekta ya uchumi Saudi Arabia amesema kuwa mikopo hiyo ni kati ya sababu za kimsingi za kuporomoka mfumo wa kiuchumi wa kibepari katika nchi za Magharibi. Ameongeza kuwa benki za Kiislamu zinauthabiti kamili katika utelekezaji shughuli zao kwa misingi ya sheria za Kiislamu.
Khaled Al-Aboodi alianza kufanya kazi Wizara ya Fedha Saudi Arabia mwaka 1982 na mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Halmashauri ya Kiislamu ya Ustawi wa Sekta Binafsi ICD. Amesema: ICD iko katika mkakati wa kuanzisha shirika la kutoa mikopo ya kununua nyumba kwa msingi wa sheria.
Halmashauri ya Kiislamu ya Ustawi wa Sekta Binafsi ni mshirika wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu IDB na huzingatia misingi ya Kiislamu katika shughuli zake za kifedha. 336733

captcha