Washiriki katika Kongamano la Kimataifa la Hijab ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Dakar, Senegal wametoa taarifa wakisema: Hijab ya mwanamke Muislamu ni nembo ya kufungamana kwake na misingi ya sheria za Kiislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Kiislamu IINA, kongamano hilo la kimataifa la Hijab ya Kiislamu lilifanyika 20-21 Disemba katika Chuo Kikuu cha Dakar na kuhudhuriwa na wanawake Waislamu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kitengo cha Dakar cha Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu Rajab Nasar, kongamano hilo limejadili athari hasi za kutovaa Hijab na udharura wa kisheria wa kulinda vazi la staha la Kiislamu Hijab na nafasi yake katika afya na utulivu wa jamii za Kiislamu.
Ameongeza kuwa, "kulinda hijab kunampa mwanamke heshima katika nyanja mbalimbali za jamii na hili litakuwa jambo lenye thamani kwa mwanamke Muislamu".
Kongamano la Kimataifa la Hijab ya Kiislamu nchini Senegal limefanyika kwa hisani ya kitengo cha Dakar cha Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu. 336674