Gazeti la Ar-Riyadh la Saudi Arabia limemnukulu Hussein Muhammad Ibrahim, Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabunge ya Kiislamu akisema: Washiriki katika mkutano wa Nicosia watajadili njia za kuhitimisha mzingiro wa Gaza ambao umekuwa ukitekelezwa na utawala ghasibu wa Israel kwa miezi kadhaa sasa.
Ameongeza kuwa, Utawala wa Kizayuni hauwezi kuvunja irada na azma ya mapambano ya taifa la Wapalestina ya kupigania ukombozi wa ardhi zao kwa kushadidisha mzingiro wa Gaza. Amesema kuwa hata kama mzingiro huo utachukua muda mrefu, lakini hatimaye Wapalestina watauvunja na kuibuka washindi.
Hassan Muhammad Ibrahim ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa mrengo wa Ikhwanul Muslimin katika bunge la Misri amenukuliwa na gazeti hilo akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuushurutisha utawala haramu wa Israel kusitisha mzingiro wake dhidi ya eneo la Gaza. 336914