IQNA

Kituo cha nuskha za hati za Imam Ali (as) chafunguliwa Najaf

12:11 - December 24, 2008
Habari ID: 1722170
Kituo cha nuskha za Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za Imam Ali bin Abi Twalib (as) na nakala za vitabu vingine vya Kiislamu kimefunguliwa katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Saut al Iraqiya, Mkurugenzi wa Maktaba ya Al Alawiya ya Najaf, Hashimi al Milani, amesema: “Katika kituo hicho kuna nuskha za Qur'ani zilizo na hati binafsi na maandiko ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) katika juzuu tatu zilizo na umri wa takriban miaka 1400”.
Ameongeza kuwa katika Kituo cha nuskha za hati za Imam Ali (as) mjini Najaf, mbali na kuwa na nuskha za Qur'ani zilizoandikwa na Mtukufu huyo, kuna nakala nyingine za Qur'ani na maandiko ya kidini ambayo ni nadra. “Athari za kituo hiki zimekusanywa kutoka maktaba za al Alawaiya, ar-Rawdha al Heidariya, al Hakim na Qashiful Ghita za mjini Najaf” amemaliza kusema Hashim al Milani . 337545

captcha