Sherehe hizo zinafanyika sambamba na kuanza mwaka mpya wa Hijria.
Shirika rasmi la habari la Imarati (WAM) limeripoti kuwa sherehe hizo zinasimamiwa na Idara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kuhamia Madina Mtume Muhammad (saw) akitokea Makka.
Mkuu wa Idara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati amesema kuwa sherehe hizo zitajumuisha ratiba kadhaa ikiwa ni pamoja na kueleza sira ya Mtume Muhammad (saw), thamani na maadili yake mema.
Vilevile maulama na wanafikra wa Kiislamu watahutubia sherehe hizo wakizungumzia tukio hilo, malengo yake na wadhifa wa Waislamu wa kufaidika na mafunzo ya sira ya Mtume Muhammad (saw). 338122