IQNA

Kongamano la kimataifa la maombolezo ya Imam Hussein kufanyika Uturuki

11:29 - December 28, 2008
Habari ID: 1723255
Huku siku za maombolezo ya kuuawa shahidi mjukuu wa Bwana Mtume (saw), Imam Hussein (as) zikikaribua, kongamano la kimataifa lenye anwani ya "Maombolezo ya Dunia ya Ashura" limepangwa kufanyika Uturuki kwa hisani ya Jumuiya ya Ja'afari.
Afisa wa Uhusiano wa Umma wa Jumuiya ya Ja'afari ya Uturuki Qasim al Jan amesema, kongamano hilo litafanyika tarehe 10 Muharram katika medani ya Ashura nchini Uturuki na kuhudhuriwa na maelfu ya wapenzi wa Imam Hussein (as) kutoka sehemu zote duniani.
Ameongeza kuwa maafisa wa serikali ya Uturuki pamoja na wageni wengine waalikwa watahudhuria kongamano hilo ambalo pia litaonyeshwa kwa njia ya moja kwa moja na televisheni ya kitaifa ya Uturuki (TRT).
Qasim al Jan amesema kuwa kongamano hilo la kimataifa la Ashura nchini Uturuki lilianza kufanyika mwaka 1990 na limekuwa likihudhuriwa kwa wingi na wapenzi wa Ahlul Bayt (as)yaani Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw) kutoka maeneo yote duniani. 338139
captcha