IQNA

Filamu ya "Maryam Mtakatifu" yaonyeshwa katika televisheni ya Zimbabwe

16:30 - December 27, 2008
Habari ID: 1723261
Sambamba na sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Nabi Issa Masih (as), filamu yenye sehemu kadhaa ya "Maryam Mtakafitu" imeonyeshwa katika televisheni ya taifa ya Zimbabwe kwa hisani ya Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Harare.
Katika mahojiano ya simu na IQNA, Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zimbabwe Muhammad Hassan Ipakchi, amesema kuwa, " filamu ya "Maryam Mtakatifu" ilivyotayarishwa na Shahriyar Bahrani ilianza kuonyeshwa 24 Disemba katika televisheni ya taifa ya Zimbabwe sambamba na kuanza sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa wa Nabi Issa (as).
Ipakchi amesema: Kwa kuzingatia kuwa Wazimbabwe wengi ni Wakristo, uonyeshaji wa filamu hivyo unalenga kukuza uhusiano wa kitamaduni kati ya Zimbabwe na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mwanadiplomasia huyo wa Iran mjini Harare amesema: Filamu ya "Maryam Mtakatifu" imeonyeshwa baada ya kumalizika filamu ya "As'habul Kahf". Hassan Ipakchi ameongeza kuwa filamu ya "As'habul Kahf" ina sehemu 20 na imeonyeshwa katika televisheni ya taifa ya Zimbabwe na kuwavutia watazamaji wengi
captcha