IQNA

Dinari inapasa kuchukua nafasi ya dola

16:48 - December 27, 2008
Habari ID: 1723283
Mahatir Muhammad, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia kwa mara nyingine tena amekariri na kutilia mkazo fikra na mtazamo wake wa kutumika dinari ya Kiislamu kama sarafu inayopasa kutumiwa katika miamala ya kibiashara na kiuchumi ya nchi za Kiislamu.
Akizungumza katika kikao kilichopewa anwani ya ‘Viwanda vya Nchi za Kiislamu’ huko nchini Yemen, Mahatir Muhammad amezitaka nchi za Kiislamu kutekeleza pendekezo lake la kutumia dinari ya Kiislamu badala ya dola ya Marekani.
Akizungumza katika kikao hicho Mahatir Muhammad amesisitiza kwamba, nchi za Kiislamu ambazo zina utajiri mkubwa wa maliasili, zinaweza kuwa na nafasi muhimu katika mfumo wa uchumi wa dunia.
Mahatir Muhammad alitoa fikra hiyo kwa mara ya kwanza katika mazungumzo yake aliyofanya hivi karibuni na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran mjini Tehran. 338440
captcha