Kwa mujibu wa IQNA mjini humo, kituo hicho cha Qur'ani kitakachojulikana kwa jina la "Hassanein", kimefunguliwa kwa hisani wa Benki ya Kiislamu ya Eika.
Hivi sasa takriban vijana 15 wa Kyrgyzstan wamesajiliwa kuanza masomo ya Qur'ani katika kituo hicho.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotufikia, msomaji Qur'ani mashuhuri wa nchi hiyo, Ustadh Muhammad atakuwa akifunza kisomo cha tajwid na hifdhi ya Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
Mkuu wa kituo hicho cha Darul Qur'an amesema: Kituo hicho kiko tayari kupokea wanafunzi wa kike na kiume wenye kati ya umri wa miaka 15 hadi 20. 338522