IQNA

Mpango wa kupambana na umaskini katika nchi za Kiislamu

11:19 - December 28, 2008
Habari ID: 1723598
Baraza la Utekelezaji la Benki ya Ustawi ya Kiislamu imebuni mpango wa kupambana na umaskini katika nchi za Kiislamu ifikapo mwaka 1430 Hijria katika kikao kilichofanyika mjini Jiddah, Saudi Arabia.
Mkuu wa Benki ya Ustawi ya Kiislamu Ahmad Muhammad Ali amesema kuwa benki hiyo imetenga dola bilioni mbili kwa ajili ya kupambana na umaskini na kutekeleza miradi ya ujenzi katika nchi za Kiislamu katika mwaka 1430 Hijria.
Ahmad Muhammad Ali ameongeza kuwa, Mfuko wa Kustawisha Mshikamano wa Kiislamu pia utatoa mkopo wa dola milioni 357 kwa nchi wanachama wa Benki ya Ustawi ya Kiislamu kwa shabaha ya kupambana na umaskini katika ulimwengu wa Kiislamu. 338817

captcha