Sayyid Sadruddin al Qubanchi amewapongeza Wakristo wote duniani kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa Miladia na akawahimiza wafuasi wa dini ya Nabii Issa Masih (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) kufaidika na mafundisho ya thamani ya mtukufu huyo na Bibi Maryam (as).
Sayyid al Qubanchi ameashiria kwamba, dini ya Kikristo haikubali ufuska na umaada unaotawala jamii za sasa za Magharibi na akasema: Wakristo wanaweza kurejea kwenye misingi ya Uislamu na mfumo wa Ahlubaiti wa Mtume kwa ajili ya kupata ufahamu sahihi wa mafundisho ya Issa Masiya (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake). Amewataka pia maaskofu wa Kikristo kubuni ratiba za kuwaongoza na kuwaelimisha Wakristo thamani halisi za dini hiyo wanapokuwa makanisani. 338682