IQNA

Balozi wa utawala wa Kizayuni Jordan akimbilia mafichoni

9:58 - December 30, 2008
Habari ID: 1724742
Kufuatia kuongezeka maandamano dhidi ya utawala wa Kizayuni huko Jordan na kushadidi hisia za kitaifa, balozi wa utawala wa Kizayuni nchini humo Jacob Ruzmir amekimbilia mafichoni kwa sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, duru za kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan zimearifu kuwa Ruzmir amejificha na hajulikani aliko.
Kwa mujibu wa duru hizo, Wajordan waliokuwa na hasira wamemiminika barabarani na mitaani kulaani jinai za utawala haramu wa Israel huko Gaza tarehe 27 Disemba na kutaka balozi huyo wa Kizayuni kufukuzwa nchini Jordan mara moja.
Takriban Wajordan 50 elfu walimiminika mitaani masaa machache baada ya jeshi katili la Kizayuni kutekeleza mashambulizi ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuwaua shahidi Wapalestina karibu 400. Maandamano kama hayo tayari yamefanyika katika maeneo 20 kote nchini Jordan. Waandamanaji wenye hasira wamelaani vikali jinai za Kizayuni huko Gaza.
Wabunge 24 kati ya 110 wa Jordan wameiandikia serikali barua rasmi wakiionya kuhusu athari mbaya za jinai za Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.
Wadadisi wa mambo wanaamini kuwa serikali ya Jordan ni kati ya serikali za nchi za Kiarabu ambao zilikuwa na habari kamili kuhusu mpango wa utawala wa Kizayuni wa kutekeleza jinai huko Gaza na kwamba nchi hiyo ilitoa ushirikiano katika jinai hiyo ya Wazayuni. 340088


captcha