Kwa mujibu wa televisheni ya al-Jazeera, ndege tano aina ya F16 za Israel jana zilifanya mashambulio ya kinyama katika maeneo ya makazi ya raia na kubomoa kabisa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza. Mara tu baada ya kutekelezwa shambulio hilo la kinyama waokoaji walifika katika eneo hilo la kusini mwa Ukanda wa Gaza na kufanya operesheni za kuwaokoa wahanga wa shambulio hilo la Wazayuni. Hakuna habari zilizoweza kupatikana kwa haraka kuhusiana na idadi ya wahanga wa shambulio hilo. 340003