IQNA

Allamah Fadhlullah kuhudhuria majlisi za maombolezo ya Muharram

8:28 - December 31, 2008
Habari ID: 1725265
Majlisi za maombolezo ya kumbukumbu kuuawa shahidi Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW na Imamu wa tatu wa Waislamu wa Kishia, Imam Hussein AS, zitafanyika katika siku 10 za mwanzo za mwezi wa Muharram na kuhutibiwa na Allamah Fadhlullah mjini Beirut.
Kwa mujibu wa mtandao wa intaneti wa Allamah Fadhlullah, majlisi na vikao hivyo vya maombolezo ya Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein AS zimeanza kufanyika tarehe Mosi Muharram kwa hisani ya ofisi ya Allamah Fadhlullah katika Masjid Hussein AS mjini Beirut.
Majlisi hizo huanza kila siku saa moja kwa wakati wa Beirut na Allamah Fadhlullah anatoa hotuba kuhusu sira na mwenendo wa Imam Hussein AS. 339535

captcha